Skip to main content

UM umeshtushwa na mauaji ya mtumishi wa WFP Usomali

UM umeshtushwa na mauaji ya mtumishi wa WFP Usomali

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeelezea kupata mshtuko mkubwa, na kuhuzunishwa, halkadhalika, kwa mauaji ya mtumishi wao mmoja anayeitwa Abdulkadir Diad Mohamed, yaliotukia Ijumaa iliopita (15/08/08) katika mji wa Dinsor, Usomali kusini.