Vikosi vya Ethiopia vyawasili Darfur kujiunga na UNAMID
Kundi la awali la Batalioni ya Wanajeshi wa Miguu 114 wa kutoka Ethiopia wanaotarajiwa kujiunga na Vikosi Mseto vya UM/UA kwa Darfur (UNAMID) limewasili kwenye mji wa jimbo la Sudan magharibi wa El-Fasher Ijumamosi tarehe 16 Agosti 2008.