Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC imeamrisha Lubanga aachiwe, halan

ICC imeamrisha Lubanga aachiwe, halan

Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) imeamrisha Thomas Lubanga Dyilo aachiwe, mtuhumiwa wa kwanza aliyekabili mashtaka kwenye Mahakama hiyo tangu ilipobuniwa. Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka, Lubanga alituhumiwa kuajiri watoto wa umri mdogo waliolazimishwa kushiriki kwenye mapigano katika eneo la Ituri katika kipindi cha baina ya 2002 hadi 2003.