Bemba amehamishwa kizuizini Hague
Kadhalika Alkhamisi ya leo aliyekuwa Naibu Raisi wa JKK, Jean-Pierre Bemba amehamishwa kutoka Burussels, Ubelgiji na kupelekwa kizuizini mjini Hague, Uholanzi yalipo makao ya Mahakama ya ICC, ambapo atawekwa akisubiri kesi. Bemba ametuhumiwa kuongoza wafuasi wa kundi lake la MLC, kuendeleza vitendo haramu vya kunajisi kimabavu raia na kuwatesa watu, katika miaka ya 2002 hadi 2003 nchini JKK.~