Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Warsha maalumu pamoja na tafrija mbalimbali zinafanyika Makao Makuu ya UM kuadhimisha miaka 10 tangu Sheria ya Roma ilipoidhinishwa na kuanzishwa Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC). KM Ban Ki-moon alisema kuanzishwa kwa Mahakama ya ICC ni moja ya mafanikio makubwa ya karne iliopita.~

Baraza la Usalama limekutana kuzingatia masuala ya kuwakinga watoto wenye umri mdogo na athari za mapigano na hatari ya kuwashirikisha kwa nguvu kwenye mapigano na vita.

Kadhalika kwenye Makao Makuu ya UM kunafanyika Kikao cha Tatu cha Mkutano wa Kimataifa Kusailia Mradi wa Utendaji wa Kuzuia, Kupambana na Kufyeka Biashara Haramu ya Silaha Ndogo Ndogo na Nyepesi katika ulimwengu.

Risala ya KM kwenye Mkutano wa Mawasiliano ya Kimataifa imezihimiza dini zote kuu za dunia kuimarisha ushirikiano mwema ili kutunza usalama na amani ya kimataifa kati yao. Mkutano unafanyika kwenye mji wa Madrid, Uspeni na umeandaliwa na Mfalme Abdullah Abdul Aziz Al-Saud wa Saudi Arabia. Alisema mizozo mingi inayodhaniwa inahusiana na masuala ya kidini vyanzo vyake vinatokana na mambo yaliokiuka itikadi tofauti. KM ametoa mwito unaopendekeza vijana wa ulimwengu wanaoamini wametengwa na jamii zao washirikishwe na viongozi wa kidini kwenye shughuli za kujenga amani.