Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yanasihi kilimo cha mihogo kiimarishwe kujikinga njaa kwa nchi masikini

FAO yanasihi kilimo cha mihogo kiimarishwe kujikinga njaa kwa nchi masikini

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limeripoti matukio ya utafiti yaliothibitisha kihakika kwamba zao la nchi za joto la mhogo lina uwezo mkubwa wa kuzisaidia nchi masikini kupata chakula na nishati kwa usalama wa kudumu, hasa yale mataifa yenye kuhatarishwa na athari za kupanda kwa kasi kwa bei za chakula na mafuta katika soko la kimataifa.

Wataalamu waliohudhuria mkutano wa sayansi ya mihogo uliofanyika Gent, Ubelgiji walitoa mwito uliohimiza nchi husika kuekeza, kwa wingi zaidi, kwenye utafiti wa kimsingi na ustawi, wa kuwasaidia wakulima masikini kuongeza mavuno ya mihogo kwenye maeneo yao. Vile vile wataalamu walipendekeza mavuno ya mihogo yatumiwe kwenye huduma za viwandani, ikijumuisha pia ile kadhia inayotumika katika kuzalisha nishati inayotokana na viumbe/vitu hai.