Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mshauri mpya wa Kijeshi kwa DPKO amewasili Makao Makuu kuanza kazi

Mshauri mpya wa Kijeshi kwa DPKO amewasili Makao Makuu kuanza kazi

Liuteni Jenerali Chikadiba Obiakor wa Nigeria, Mshauri wa Masuala ya Kijeshi katika Idara ya UM Kuhusu Operesheni za Ulinzi wa Amani (DPKO) amewasili New York Alkhamisi kuanza kazi. Jenerali Obiakor amedhaminiwa madaraka ya kuishauri Idara ya DPKO juu ya masuala yote ya kijeshi yanayofungamana na shughuli za ulinzi amani za UM.

wanaume na wanawake

walioenezwa sehemu kadha wa kadha za ulimwengu. Jenerali Obiakor aliyejiunga na Jeshi la Nigeria 1973, atakuwa mshauri mpya wa kwanza wa masuala ya kijeshi katika DPKO kupewa cheo cha Msaidizi KM au ASG.