Mjumbe wa UM amekutana kwa mazungumzo na Raisi wa Zimbabwe

Mjumbe wa UM amekutana kwa mazungumzo na Raisi wa Zimbabwe

Haile Menkerios, KM Mdogo juu ya Masuala ya Kisiasa ambaye aliwasili Zimbabwe mapema wiki hii, anaendelea na ziara yake nchini humo. Ijumanne alipata fursa ya kufanya mazungumzo rasmi na Rasisi Robert Mugabe ambapo walizingatia mazingira ya kisiasa yaliotanda nchini kwa sasa, kabla ya duru ya pili ya uchaguzi ujao utakaofanyika tarehe 27 Juni. Menkerios alijaribu kusailia ni mchango wa aina gani Zimbabwe itahitajia kutoka UM kusaidia kudhibiti bora mambo nchini.

Menkerios aliwaambia waandishi habari Zimbabwe ya kwamba UM itaunga mkono juhudi zote za Jumuiya ya Maendeleo ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika (SADC)kukuza uwezo wa kuendeleza uangalizi bora wakati wa uchaguzi.