Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa Haki za Binadamu anapinga upigaji marufuku Ofisa wa UM Zimbabwe

Mkuu wa Haki za Binadamu anapinga upigaji marufuku Ofisa wa UM Zimbabwe

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Louise Arbour, katika mkutano na waandishi habari Geneva, hii leo, amelaumu kitendo cha kufukuzwa Zimbabwe ofisa wa UM anayehusika na haki za binadamu. Alisema Arbour hatua hiyo ya Serikali ya Zimbabwe ni ya "kusikitisha, na humaanisha imeamua kufuata mwelekeo uliochaguliwa na serikali, wenye azma ya kutoshirikiana katu na taasisi kadha wa kadha za kimataifa ziliopo nchini."~

Ofisa aliyefukuzwa Zimbabwe anafanya kazi na Kamisheni ya UM juu ya Haki za Binadamu iliopo Geneva, na alikuwa akifanya ziara ya kawaida ambapo hushirikiana na Timu ya Watumishi Wakaazi wa UM na mashirika yasio ya kiserikali katika uchunguzi wa masuala yanayohusu namna haki za binadamu zinavyotekelezwa Zimbabwe. Ofisa huyo aliamrishwa kuihama nchini halan Ijumanne kwa kisingizio kwamba Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu (OHCHR)ilishindwa kupeleka ombi la kupatiwa idhini ya kuingia nchini kwa wakati. Ofisi ya OHCHR imeripoti kwamba ilifuata taratibu za kawaida na wenye madaraka Zimbabwe na ingelipendelea kuona mfanyakazi wao anarejeshwa nchini kukamilisha majukumu yake.