Skip to main content

Wajumbe wa Kimataifa wakutana kushauriana juu ya Usomali

Wajumbe wa Kimataifa wakutana kushauriana juu ya Usomali

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Oul-Abdallah Ijumanne alikutana mjini Nairobi na wajumbe wa Umoja wa Afrika (AU), Umoja wa Ulaya (EU), Marekani, Norway na Jumuiya za Nchi za Kiarabu ambapo walishauriana taratibu za kuhamasisha Serikali ya Mpito ya Usomali pamoja na Shirikisho la Ukombozi Mardufu la Usomali kutekeleza, kwa wakati, yale Maafikiano ya Djibouti.