OHRC inaitaka Misri isitishe kufukuza nchi WaEritrea
Louise Arbour, Kamishna Mkuu wa Ofisi ya UM juu ya Haki za Binadamu (OHRC), ameripoti "kushtushwa sana" na taarifa zinazothibitisha ya kuwa katika siku za karibuni taifa la Misri limefukuza na kuondosha nchini wahamiaji 700 wa kutoka Eritrea, walikuweko nchini humo wakisubiri jawabu ya maombi yao ya kupatiwa hifadhi ya kisiasa.