UNDOC imefadhiliwa dola milioni 3 na OPEC kupanua tiba dhidi ya UKIMWI
Ofisi ya UM juu ya Udhibiti wa Uhalifu na Madawa ya Kulevya (UNDOC) iliopo Vienna, Austria wiki hii ilifadhiliwa msaada wa dola milioni 3 kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Shirika la OPEC, fedha ambazo zinatarajiwa kutumiwa kupanua huduma kinga za tiba dhidi ya UKIMWI, matibabu yanayojulikaa kama Tiba ya Awamu ya Pili au Treatnet II. Msaada huu utagawanywa kwenye mataifa manne ya Amerika ya Latina, nchi nne ziliopo Kusini Mashariki ya Asia na vile vile mataifa manne ya Afrika kusini mwa Sahara, ikijumuisha Kenya, Sierra Leone, Tanzania na Zambia.