Djibouti kuomba msaada wa BU kuzuia uhasama mipakani na Ethiopia
Jamii ya kimataifa imeingiwa na wahka mkuu kutokana na ripoti zilizopokewa karibuni juu ya kufura kwa hali ya wasiwasi mipakani baina ya Djibouti na Eritrea. Kwa mujibu wa taarifa hizo, Djibouti imetuma barua rasmi kwa Raisi wa Baraza la Usalama iliodai kuwa imeshuhudia kuongezeka kwa idadi ya vikosi vya Eritrea mipakani. Kutokana na sababu hizo Djibouti ilisema ndipo ilipolazimika kuliomba Baraza la Usalama liitishe kikao cha haraka kuzingatia hatua za dharura zitakazosaidia kuzuia mikwaruzano kuzuka kati ya mataifa haya jirani yaliopo katika Pembe ya Afrika.