Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani katika Sierra Leone inazingatiwa na Baraza la Usalama

Amani katika Sierra Leone inazingatiwa na Baraza la Usalama

Baraza la Usalama limekutana Ijumatano asubuhi kuzingatia ripoti ya KM kuhusu maendeleo ya shughuli za amani katika Sierra Leone. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya KM, iliotolewa rasmi mwanzo wa wiki, ilisisitizwa ya kuwa operesheni za UM zimeiwezesha Sierra Leone kupata "maendeleo muhimu" kabisa, takriban katika sehemu zote za taifa, hasa katika zile shughuli za kuisaidia Serikali kudumisha amani.