Huduma za kiutu za UM zaendelea Myanmar
UM unaendelea kuimarisha mchango wake kwenye huduma mbalimbali za kuwasaidia waathiriwa wa Kimbunga Nargis kilichopiga Myanmar mwisho wa wiki iliopita, na kusababisha uharibifu mkubwa kabisa nchini humo. Mwandishi habari wa Redio ya UM, Carlos Araujo alimhoji Richard Horsey, Msemaji wa Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA), aliopo Bangkok, Thailand kuhusu hali halisi katika Myanmar, na kuzingatia juhudi za mashirika ya UM kwenye eneo la maafa.
Sikiliza taarifa kamili kwenye idhaa ya mtandao.