Skip to main content

Ajenda ya Aprili kuzingatiwa na Baraza la Usalama, uhusiano bora na UA watiliwa mkazo

Ajenda ya Aprili kuzingatiwa na Baraza la Usalama, uhusiano bora na UA watiliwa mkazo

Ijumatano asubuhi Baraza la Usalama (BU) chini ya Uraisi wa Balozi wa Afrika ya Kusini Dumisani Kumalo lilikutana kwa kushauriana kuhusu ajenda ya kazi kwa mwezi Aprili. Baada ya mamshauriano hayo Balozi Kumalo alikutana na waandishi habari wa kimataifa katika Makao Makuu ambapo alibainisha ajenda ya Baraza la Usalama kwa mwezi huu imenuia zaidi kuimarisha uhusiano mwema baina ya UM na mashirika ya kimaeneo, hususan Umoja wa Afrika. ~~