Skip to main content

Rais wa BK anasema MDGs yatakamilishwa kwa wakati pakishirikiana mataifa tajiri na masikini

Rais wa BK anasema MDGs yatakamilishwa kwa wakati pakishirikiana mataifa tajiri na masikini

Raisi wa Baraza Kuu (BK) Srgjan Kerim Ijumatano aliwaambia wajumbe waliohudhuria majadiliano yaliofanyika Makao Makuu, kuzingatia uwezekano wa kuyakamilisha Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) katika 2015, kwamba tunaweza kuyakamilisha haya Malengo ya Milenia kwa wakati pindi Mataifa tajiri na masikini yatashirikiana kidhati, kipamoja, kuzitekeleza ahadi zao walizotoa hapo kabla. Kadhia hii ikikamilishwa, alisisitiza Raisi wa Baraza Kuu itaharakisha pakubwa maendeleo ya kiuchumi na jamii kwenye maeneo husika, hali ambayo itasaidia pia kupunguzu ufukara na umasikini.