Skip to main content

UM yaadhimisha Siku ya Kukumbushana Hatari ya Mabomu ya Kufukia

UM yaadhimisha Siku ya Kukumbushana Hatari ya Mabomu ya Kufukia

Tarehe 04 Aprili kila mwaka huheshimiwa kimataifa kuwa ni Siku ya Kukumbushana Uovu na Hatari ya Mabomu Yaliotegwa Ardhini.

Timu ya wataalamu kutoka mashirika 14 ya UM – ikijumuisha pia wale wataalamu wanaohudumia shughuli za kufyeka na kuondoa mabomu yaliotegwa ardhini – wanaendelea hivi sasa kuongoza miradi kadha wa kadha ya kufyeka silaha hizi katika nchi na maeneo 43 yaliozagaa katika sehemu mbalimbali za ulimwengu.