Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubaguzi dhidi ya wanawake haujakomeshwa kitambo kufuatia ahadi za Beijing, OHCHR inaonya

Ubaguzi dhidi ya wanawake haujakomeshwa kitambo kufuatia ahadi za Beijing, OHCHR inaonya

Uchunguzi uliodhaminiwa na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu (OHCHR), kuhusu utekelezaji wa ahadi za Mkutano wa Beijing wa 1994 za kukomesha ubaguzi dhidi ya wanawake, umethibitisha kwamba nchi kadha wa kadha, katika sehemu mbalimbali za dunia, bado zinaendelea kudumisha sheria zenye kubagua wanawake. Matokeo ya yalisisitiza kwamba ahadi za marudio ziliotolewa na Mataifa Wanachama kubatilisha na kusahihisha zile sheria zenye ubaguzi wa kijinsia zimeonekana kupwelewa katika sehemu nyingi za dunia.

Mathalan, zile sheria za ndoa, hususan katika mataifa ya Afrika, bado zinaendelea kubagua watoto wa kike. Mwandishi wa ripoti ya uchunguzi uliodhaminiwa na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ni Dktr Farida Banda wa Chuo Kikuu cha London juu ya Taaluma ya Pande za Asia na Afrika (SOAS).

Sikiliza dokezo ya fafanuzi za Dktr Farida katika idhaa ya mtandao.