Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walioathiriwa kiakili Kenya na machafuko ya uchaguzi kusaidiwa tiba na IOM

Walioathiriwa kiakili Kenya na machafuko ya uchaguzi kusaidiwa tiba na IOM

Shirika la Kimataifa kuhusu Uhamaji (IOM) limeripoti kwamba limepokea kutoka Serikali ya Norway msaada wa dola 504,000, fedha zitakazotumiwa kuwasaidia raia wa Kenya wanaokisiwa 200,000, kupata tiba ya maradhi ya akili. Umma huu inasemekana ulidhuriwa kiakili kufuatia machafuko yaliotukia nchini baada ya uchaguzi wa Disemba mwaka jana.~