Skip to main content

KM ahutubia Mhadhara wa Geneva, atathminia athari za mfumko wa bei za chakula duniani

KM ahutubia Mhadhara wa Geneva, atathminia athari za mfumko wa bei za chakula duniani

Ijumanne KM Ban Ki-moon alihutubia, kwa mara ya awali, mhadhara mpya unaojulikana kama Mhadhara wa Geneva, ambapo alizungumzia hatari inayokabili umma wa kimataifa kutokana na kuenea, kwa mapana na marefu, kwa lile tatizo la kupanda kwa kasi kwa bei za chakula duniani.

Mhadhara wa Geneva umekusudiwa kuwasilisha mfululizo wa mihadhara ya hadhi ya juu, itakayosaidia kuamsha hisia za fungu kubwa la wakazi wa Geneva kuhusu masuala muhimu yanayoukabili ulimwengu, kwa ujumla, na kuzingatia zaidi mchango wa watu binafsi katika kuyatatua matatizo hayo.