Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kwamba matokeo ya utafiti wa karibuni yamethibitisha asilimia 4 tu ya wahamiaji wa Iraq waliopo Syria, waliohajiri makwao kwa sababu ya vurugu wapo tayari kurejea nchini kwao. Asilimia 95 ya wahamiaji hawa waliihama Iraq kutokana na vitisho pamoja na ukosefu wa usalama kijumla.

Kwenye kikao cha kimataifa kinachofanyika wiki hii mjini Paris, Ufaransa kuzingatia hali ya wahamiaji wa Kifalastina ulimwenguni, risala ya KM iliosomwa na Angela Kane, Kaimu Mshauri juu ya Masuala ya Kisiasa, ilitahadharisha ya kuwa penye ukosefu wa suluhu inayoridhisha, na ya haki, kuhusu suala la wahamiaji wa KiFalastina tutashindwa kuwasilisha amani ya kudumu katika eneo zima la Mashariki ya Kati.