Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

'Ukame mkali wazagaa Usomali', kuonya UM

'Ukame mkali wazagaa Usomali', kuonya UM

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohudumia misaada ya kiutu, ikijumuisha shirika linalohusika na maendeleo ya watoto UNICEF, miradi ya chakula, WFP, na lile linalohudumia wahamiaji, UNHCR, pamoja na jumuiya zisio za kiserekali hivi sasa wameamua kuongeza michango maridhawa, ya kihali, kufadhilia eneo la Usomali kati, ambapo inasemekana ukame mbaya umetanda kwa wingi, na unapalilia ufukara kwa jamii ambazo zimekabiliwa na upungufu mkubwa wa maji pamoja na uhaba wa malisho kwa wanyama wa mifugo.