Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM alisihi Baraza la Haki za Binadamu kuyakamilisha matarajio ya umma

KM alisihi Baraza la Haki za Binadamu kuyakamilisha matarajio ya umma

Ijumatatu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alihutubia rasmi mjini Geneva kikao cha cha saba cha Baraza la Haki za Binadamu. Kwenye hotuba yake ya ufunguzi alisema ni wajibu wa Baraza hilo, kuhakikisha kazi zake zinaambatana na matarajio waliyonayo jamii ya kimataifa juu ya taasisi hiyo.

Alisisitiza kila taifa, hata likiwa na nguvu zilizovuka kawaida, ni lazima lichunguzwe kama libnnatekeleza na kuheshimu haki za binadamu kama inavyotakiwa.