BU haitoidhinisha utumiaji nguvu dhidi ya shughuli za nyuklia za Iran
Balozi Vitaly Churkin wa Urusi, Raisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Machi, aliwaambia wanahabari wa kimataifa Ijumanne kwamba vikwazo vilioekewa Iran kwa kutositisha usafishaji wa maadini ya yuraniamu, ambayo hutumiwa kuzalisha nishati ya nyuklia, haimaanishi hata kidogo Baraza hilo litaunga mkono matumizi ya nguvu za kijeshi dhidi ya Iran, na kuilazimisha kuyatekeleza mapendekezo ya maazimio yanayohusu tuhuma za kutengeneza silaha za nyuklia.