Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Operesheni za awali za Polisi wa UNAMID zaanzishwa rasmi Darfur Kaskazini

Operesheni za awali za Polisi wa UNAMID zaanzishwa rasmi Darfur Kaskazini

Ikiwa miongoni mwa juhudi za kuimarisha ushirikiano bora na hali ya kuaminiana, baina ya Umoja wa Mataifa pamoja na wenyeji na polisi katika Darfur, operesheni za kwanza za polisi wa Vikosi Mseto vya UM/UA kwa Darfur (UNAMID) zilianzishwa mapema wiki hii katika sehemu za Darfur ya Kaskazini kujenga imani. Eneo hili linasimamiwa na kundi la Mini Minawi, tawi la wanamgambo waasi wa SLA.

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa ofisa wa polisi 1,600 kutoka nchi wanachama 32 – wakijumuisha pia polisi wanawake 252 – hivi sasa wanatumikia Shirika la UNAMID katika Darfur.