Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinzi wa UNMEE waondolewa Asmara na kupelekwa kwenye uhamisho wa muda

Walinzi wa UNMEE waondolewa Asmara na kupelekwa kwenye uhamisho wa muda

Ijumanne kundi la kwanza la wanajeshi wa Jordan 50 wanaohudumia ulinzi wa amani mipakani kati ya Eritrea/Ethiopia, yaani wanajeshi wa UNMEE, walisafirishwa na ndege za Umoja wa Mataifa kutoka mji mkuu wa Asmara, Eritrea na kupelekwa kwenye uhamisho wa muda, wakati wakisubiri uamuzi wa Baraza la Usalama juu ya hatua za kuchukuliwa kuendeleza operesheni zao mipakani katika siku za usoni. Umoja wa Mataifa umelazimika, kwa sasa, kuwahamisha walinzi wa amani wa UNMEE nje ya Eritrea kwa sababu walinyimwa nishati na wenye madaraka, inayohitajika kuendeleza shughuli zake mipakani.