Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC kuendesha kesi mbili kwa pamoja za watuhumiwa wa jinai ya vita katika JKK

ICC kuendesha kesi mbili kwa pamoja za watuhumiwa wa jinai ya vita katika JKK

Majaji wa Mahakama ya UM juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) iliopo mjini Hague, Uholanzi wameamua kuendesha kesi mbili, baadaye mwaka huu, kwa wakati mmoja, zinazowahusu viongozi wawili waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK), yaani Germain Katanga na Mathieu Ngudjolo Chui, ambao walituhumiwa kuendeleza makosa ya vita na jinai dhidi ya utu katika eneo la mashariki ya taifa hilo, mnamo 2003. Miongoni mwa mashitaka waliokabiliwa nayo watuhumiwa hawa ni pamoja na kushtakiwa kushiriki kwenye mauaji ya mamia ya watu na kuendeleza karaha ya kunajisi wanawake kimabavu katika jimbo la Ituri.~