Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulio ya wabunge Burundi yamtia wasiwasi KM

Mashambulio ya wabunge Burundi yamtia wasiwasi KM

Mashambulio ya vijikombora vidogo vilivyorushwa mwisho wa wiki kwenye nyumba za wabunge wanne mjini Bujumbura, Burundi ni tukio “liliomshtusha sana” KM Ban Ki-moon na kumlazimisha kutoa mwito maalumu, kwa kupitia Msemaji wake Michele Montas, unaowaomba wenye madaraka nchini kufanya kila wawezalo kuhakikisha waliofanya kosa hilo wanatiwa mbaroni na wanafikishwa mahakamani bila ya kuchelewa.~~~