Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miriam Makeba azuru wanawake walioathiriwa wa machafuko katika JKK

Miriam Makeba azuru wanawake walioathiriwa wa machafuko katika JKK

Miriam Makeba, mwanaharakati na mwimbaji mashuhuri wa Afrika Kusini, ambaye ni Balozi Mhisani wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) wiki hii anazuru Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK). Alipokuwepo Kinshasa aliwaambia waandishi habari ya kuwa wale wanawake walionusurika kimaisha, baada ya kunajisiwa kimabavu kutokana na mazingira ya vita na uhasama, wanawake hawa wanahitajia kusaidiwa kihali kupatiwa tiba ifaayo, na pia kusaidiwa kwa mali ilivyokuwa asilimia 80 ya aila ziliopo kaka JKK hutegemea pato linalochunmwa na wanawake kuendesha maisha.