Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wapatanishi wa UM/UA kwa Darfur watakutana Geneva wiki ijayo kufufua mpango wa amani

Wapatanishi wa UM/UA kwa Darfur watakutana Geneva wiki ijayo kufufua mpango wa amani

Wapatanishi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwa Darfur, yaani Salim Ahmed Salim na Jan Eliasson wanatarajiwa kukutana wiki ijayo mjini Geneva, Uswiss kuendeleza mashauriano, yasio rasmi, pamoja na waangalizi wa kimataifa na pia wadau wa eneo la mgogoro katika Sudan, ikiwa miongoni mwa juhudi za kimataifa katika kusukuma mbele utekelezaji wa Mpango wa Amani kwa Darfur.