Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chad na Sudan watiliana sahihi mapatano ya kutochokozana

Chad na Sudan watiliana sahihi mapatano ya kutochokozana

Raisi Omar al-Bashir wa Sudan pamoja na Raisi Idriss Deby wa Chad walitiliana sahihi mkataba uliokubali utaratibu wa kusitisha uchokozi na mashambulio kati ya mataifa yao jirani. Mwafaka huu ulifikiwa na kutiwa sahihi kwenye saa za usiku wa Alkhamisi, katika mji wa Dakar, Senegal ambako viongozi hawo wawili walikuwa wanahudhuria Mkutano wa Umoja wa Nchi za KiIslam (OIC).