Skip to main content

UM imeripoti wahamiaji wa IDPs Kenya wamegoma kurejea makwao kukhofia usalama usio hakika

UM imeripoti wahamiaji wa IDPs Kenya wamegoma kurejea makwao kukhofia usalama usio hakika

Naibu Msemaji wa KM, Marie Okabe, kwenye mkutano na waandishi habari hapa Makao Makuu Alkhamisi alibainisha kwamba wale raia wa Kenya wanaoishi kwenye kambi za wahamiaji wa ndani ya nchi (IDPs) baada ya kuongo’lewa makwao, kufuatia matokeo ya uchaguzi, umma huu haupo tayari kurejea kwenye maeneo yao kwa sababu ya ukosefu wa usalama.~