Uchanganuzi batini wa Tanzania juu ya kikao cha Kamisheni ya Maendeleo ya Jamii

25 Machi 2008

Kuanzia tarehe 06 mpaka 15 Februari wawakilishi wanachama wa Kamisheni juu ya Maendeleo ya Jamii walikusanyika kwenye Makao Makuu ya UM mjini New York, kuhudhuria kikao cha mwaka, cha arobaini na sita, ambapo walizingatia mada maalumu zenye kuhusu masuala yanayoambatana na huduma za jamii, mathalan, taratibu za kukuza ajira, nidhamu ya kukidhi vyema mahitaji ya umma unaozeeka pamoja na kusailia matatizo yaliowakabili walemavu ulimwenguni.

Ernest Ndimbo, Mkurugenzi wa Ajira kwenye Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Watoto katika Tanzania alikuwa miongoni mwa wajumbe waliohudhuria kikao cha mwaka huu cha Kamisheni ya Maendeleo ya Jamii, edio ya UM ilipata fursa ya kufanya mahojiano naye kwenye studio zetu ziliopo Makao Makuu.

Sikiliza uchambuzi kamili wa Ndimbo, kuhusu kikao cha mwaka huu, kwenye idhaa ya mtandao.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter