Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa UM aelezea athari za vurugu Kenya katika Baraza la Usalama

Afisa wa UM aelezea athari za vurugu Kenya katika Baraza la Usalama

Baraza la Usalama lilikutana kwenye kikao maalumu cha faragha kusailia hali nchini Kenya. Makamu KM juu ya Masuala ya Kisiasa, B. Lynn Pascoe aliwasilisha taarifa iliyoelezea kihakika hali ilivyo, ambapo inasemekana watu robo milioni walin’golewa makwao.

Baada ya hapo Pascoe alikutana na waandishi habari na kusema kwamba “makundi yote yaliofarakana yanawajibika kufanya kazi pamoja” ili kukomesha vurugu liliotanda nchini mwao, haraka iwezekanavyo.