Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

George Clooney ameteuliwa rasmi na UM kuhubiri amani

George Clooney ameteuliwa rasmi na UM kuhubiri amani

Mwigizaji Maarufu wa Michezo ya Sinema Marekani, George Clooney, ameteuliwa rasmi wiki hii na KM kuwa Mjumbe Maalumu wa Kuhubiri Amani.

Alipokuwepo Makao Makuu Alkhamisi alikutana na waandishi habari wa kimataifa na alinasihi ya kuwa wakati umewadia kwa nchi wanachama kuharakisha mchango wa vikosi mseto vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kwa Darfur (UNAMID), ili kuimarisha utulivu na amani, na pindi mataifa yatashindwa kuyatekeleza hayo watalazimika “kutumia uungwana na kuwarudisha wanajeshi wote hawo makwao.”