Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM kulaani vikali uvamizi wa vikosi vya serikali kwenye majengo ya UM Mogadishu

KM kulaani vikali uvamizi wa vikosi vya serikali kwenye majengo ya UM Mogadishu

KM Ban Ki-moon amelaani vikali uvamizi wa kimabavu, na ulio haramu, wa askari karibu 60 wa vikosi vya usalama vya Serikali ya Usomali,uliofanyika kwenye majengo ya UM mjini Mogadishu tarehe 17 Oktoba. Tuliarifiwa wanajeshi hao walimshikia bunduki Idris Osman, ofisa wa Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) na kumkamata na baadaye kumpeleka kizuizini. Kutokana na tukio hili WFP imelazimika kusitisha, kwa sasa, operesheni zake za kugawa chakula kwa watu muhitaji 75,000 katika eneo hilo.