UM kusaidia polisi wa Liberia kufikia viwango vya kimataifa vya haki za binadam.
Mjumbe maalum wa UM huko Liberia amekabidhi kwa Kikosi cha Polisi cha Taifa, jengo lililo karabatiwa upya la kuwaweka wafungu kulingana na masharti muhimu kabisa ya viwango vya kimataifa vya haki za binadam.
Wakati wa sherehe za kukabidhi jengo hilo mjumbe maalum wa Katibu Mkuu, Bw Alan Doss alisisitiza kwamba, afisi ya UM, UNMIL itaendelea kuisaidia Kikosi cha Polisi cha Taifa kua taasisi yenye vifaa vya kutosha na ujuzi wa hali ya juu ya uwongozi. Alihimiza kikosi cha polisi kulinda haki za binadam pamoja na za wafungwa. Akimuongoza Bw Doss, Inspekta mkuu wa Polisi Bi Beatrice Monah Sieh, alieleza shukurani zake kwa UNMIL na serekali ya Uholanzi kwa kukamilisha kazi za kituo hicho cha kuwatia watu kizuizini hadi kufunguliwa mashtaka.