Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM na UNMIS walaani mauaji ya wanajeshi wa AMIS katika Darfur

KM na UNMIS walaani mauaji ya wanajeshi wa AMIS katika Darfur

KM Ban Ki-moon amearifu kuhuzunishwa na mauaji ya kihorera ya wanajeshi watano wa vikosi vya ulinzi wa amani vya Umoja wa Afrika (AMIS) yaliyofanyika Ijumapili iliopita katika eneo la Um Baru, kilomita 220 kutoka El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur ya Kaskazini.

Kadhalika, Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika Sudan (UNMIS) limelaumu vikali mauaji hayo, na vile vile kulaani shambulio la helikopta ya AU iliokuwa ikielekea El Fasher, kutokea Zengei, Darfur ya Magharibi ambayo ilikuwa imepakia Naibu Kamanda wa vikosi vya AMIS na maofisa waandamizi. UM unawataka wenye madaraka wafanyishe uchunguzi wa dharura ili kuwashika wale walioendeleza jinai hiyo na, hatimaye, kuwafikisha mahakamani kukabili haki, haraka iwezekanavyo.