Hapa na pale
Antonio Guterres, Kamishna Mkuu was Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR, alipokuwa ziarani Mashariki ya Kati wiki hii, aliahidi kuwa atapeleka Iraq maofisa zaidi wa shirika lake kuwasaidia kihali wale WaIraki karibu milioni 4 waliong’olewa makwao kutokana na vurugu lilioshtadi nchini mwao.~
Kiyotaka Akasaka, mwanadiplomasiya wa Ujapani mapema ameapishwa mwanzo wa wiki kuwa Naibu KM wa Mawasiliano na Habari za Umma, yaani mkuu mpya atakayeongoza Idara ya Habari ya UM (DPI).