Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuimarisha huduma mseto kwa Darfur

UM kuimarisha huduma mseto kwa Darfur

Mkutano wa sita wa Makundi Matatu ya Ushauri ulifanyika mjini Khartoum wiki hii kuzingatia usimamizi bora wa mpango wa amani katika Darfur. Mpango huu unahusisha Serekali ya Sudan, Umoja wa Mataifa (UM) na pia Umoja wa Nchi Huru za Afrika (AU). Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani kwa Sudan (UNMIS) liliripoti mkutanoni ya kwamba UM umeshaajiri maofisa waandalizi wa kijeshi 21 pamoja na wafanyakazi wa kiraia 11, ambao wapo Khartoum wakisubiri kupelekwa Darfur kuwasaidia walinzi wa amani wa AU, wakiwa sehemu ya mwafaka wa Furushi Hafifu la Msaada wa vikosi vya mseto vinavyohitajika kuimarisha utulivu na amani katika Darfur.