Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Louise Arbour, Kamishna Mkuu juu ya Haki za Kibinadamu alifanya mahojiano wiki hii na wawakilishi wa vyombo vya habari waliopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UM) ambapo alionya kwamba licha ya kupatikana maendeleo karibuni katika ulinzi wa haki za kibinadamu, hususan katika mwaka huu - na kutoa mfano wa kupitishwa ule mkataba wa kupinga tabia ya kutorosha watu na kuwaangamiza - hata hivyo, yeye binafsi, alisema, anaamini bado mchango mkubwa ziada unahitajika katika sehemu nyengine za maamirisho ya haki za kibinadamu ulimwenguni, hususan katika juhudi za kukomesha kile alichokiita “msiba wa baa” la unyanyasaji na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake.~

- Kuanzia Alkhamisi, Afrika ya Kusini imedhaminiwa madaraka ya uraisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Machi.