Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP inabashiria tatizo la njaa kusini ya Afrika

WFP inabashiria tatizo la njaa kusini ya Afrika

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kuingiwa na wasiwasi unaoashiria kufumka, kwa mara nyengine tena katika maeneo ya kusini ya Afrika, janga la njaa kwa sababu ya kujiri karibuni kwa hali ya hewa ya kigeugeu. Hali hii imezusha ukame na mafuriko ambayo yaliharibu mavuno na kuathiri mamilioni ya watu watakaotegemea kusaidiwa chakula na jamii ya kimataifa kwa mwaka mzima.

Kwa mujibu wa WFP baadhi ya sehemu za Angola, Bukini, Msumbiji, Namibia na Zambia ziligharikishwa vibaya sana na mafuriko haribifu yalioangamiza makumi elfu ya hekta za mazao katika majira ya kupanda mbegu. Ama Lesotho, Namibia, Msumbiji kusini, na pia katika sehemu kubwa ya ardhi ya Swaziland na katika eneo la mazao liliofunika Zimbabwe, kwa ujumla sehemu hizi zote zimeathiriwa na ukame wa muda mrefu ulioangamiza mazao na kudidimiza maendeleo ya kilimo. punguza vibaya kutoka na muhimu ioni ya wakazi wa kusini ya Afrika, kwa mwaka huu.

Shirika la WFP sasa hivi linahudumia chakula watu milioni 4.3 kusini ya Afrika, na linahitajia kufadhiliwa kidharura mchango wa dola karibu milioni 100 kumudu operesheni zake kwa mwaka huu.