Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uvamizi wa polisi wa Mahakama Kuu Uganda umelaumiwa na UM

Uvamizi wa polisi wa Mahakama Kuu Uganda umelaumiwa na UM

Ofisi ya UM juu ya Haki za Kibinadamu nchini Uganda imetoa mwito maalumu kwa Serekali kuheshimu uhuru wa mahakama. Mwito huu ulitolewa baada ya askari polisi wenye silaha walipovamia Mahakama Kuu mjini Kamapala, hivi majuzi, na kuwatia mbaroni, kwa mara nyengine tena, wale raia wafuasi wa Kundi la People\'s Redemption Army (PRA), baada ya raia hao kuachiwa kwa dhamana na Mahakama Kuu mjini Kampala. Ofisi ya UM imesisitiza ya kuwa "mahakama ilio huru kuendeleza shughuli zake ndio ufunguo hakika wa kuimarisha utaratibu wa kufuata sheria katika jamii huru ya kidemokrasia."