Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-Moon ana matumaini amani kurejea tena Uganda kaskazini

Ban Ki-Moon ana matumaini amani kurejea tena Uganda kaskazini

KM Ban ameripoti wiki kuwa na mataraji ya kutia moyo kwamba hali ya utulivu na amani itarejea tena katika Uganda ya Kaskazini, kutokana na juhudi za Joaquim Chissano, Mjumbe Maalumu wa KM kwa maeneo yalioathirika na mapigano na waasi wa kundi la LRA.

KM amefurahika kwamba viongozi wa makundi yote yaliohudhuria mazungumzo hayo, akiwemo kiongozi wa LRA Joseph Kony, wamesisitiza kuwa wanataka amani na wapo tayari kuongeza vifungu ziada kwenye yale Mapatano ya Kusitisha Uhasama, ili kuhakikisha utulivu unarudishwa na amani kuwasilishwa. Makundi haya husika yote yameyaidhinisha Mapatano ya Kusitisha Uhasama.