Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji wa haki DRC : zaidi ya askari 50 wahukumiwa

Ukiukwaji wa haki DRC : zaidi ya askari 50 wahukumiwa

Ofisi ya Haki za Binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo DRC imesema kwamba jumla ya wanajeshi na polisi 56 nchini humo walihukumiwa mwezi uliopita kwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo ukatili wa kingono. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte

(Taarifa ya Priscilla)

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu nchini DRC kwenye ripoti yake ya mwezi wa Aprili, iliyotolewa leo imekaribisha ripoti hiyo.

Miongoni mwa visa hivyo ni uhalifu wa kingono, mauaji yaliyo nje ya mfumo wa kisheria, ukiukwaji wa haki za kisiasa, uhalifu dhidi ya watoto.

Ofisi hiyo imeorodhesha visa 366 vya ukiukwaji wa haki za binadamu mwezi Aprili nchini humo, ikilinganishwa na 410 mwezi wa Machi, asilimia 52 ya visa hivyo vikitekelezwa na maafisa wa serikali.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, majimbo ya mashariki mwa nchi yameathirika zaidi na uhalifu huo.