Ujasiriamali katika ICT ni muarabaini wa changamoto za sasa- ITU

Ujasiriamali katika ICT ni muarabaini wa changamoto za sasa- ITU

Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mawasiliano na Habari, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka teknolojia ya habari na mawasiliano, ICT iharakishe maendeleo ya binadamu, izibe pengo la dijitali na kuongeza maarifa.

Katika ujumbe wake Ban amesema katika teknolojia hizo zina uwezo wa kutatua mabadiliko ya tabianchi, afya, njaa, umasikini na changamoto zingine za kimataifa, hivyo ametaka serikali na sekta binafsi waendeleze teknolojia mpya ambazo zina mafanikio ya kudumu kwa jamii.

Houlin Zhao ni Katibu Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Duniani, ITU na anasema hilo linawezekana hivyo….

(Sauti ya Houlin)

“Ujasiriamali katika ICT unalenga kuleta mabadiliko kwenye jamii. Tunahitaji utaalamu, ubunifu na uwekezaji ili kufanikisha malengo yetu ya pamoja ya maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.”