Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lugha ya Kirusi yakataliwa kama moja ya lugha za taifa nchini Latvia

Lugha ya Kirusi yakataliwa kama moja ya lugha za taifa nchini Latvia

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa wa masuala kuhusu jamii ndogo Rita Izsak ameitaka serikali ya Latvia kuhakikisha kuwa imelinda haki za jamii ndogo zinazotumia lugha ya kirusi na kufanya mazungumzo baada ya kura ya maoni ya Februari 18 iliyokataa pendekezo la kuitambua lugha ya kirusi kama lugha ya pili ya taifa.

Bi Izsak amesema kuwa kura hiyo ya maoni haistahili kuonekana kama mafanikio kwa jamii moja dhidi ya nyingine lakini inastahili kuonekana kama mwanzo wa mazungumzo kuhusu haki za jamii ndogo nchini Latvia. George Njogopa na taarifa kamili.