Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukaji wa haki za binadamu katika DRC wataharakisha MONUC

Ukiukaji wa haki za binadamu katika DRC wataharakisha MONUC

Shirika la MONUC linalohusika na Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK/DRC)limeripoti kuingiwa na wasiwasi mkuu kuhusu kuendelea kwa ukiukaji wa haki za binadamu nchini. Kwa mujibu wa taarifa za Ofisi ya MONUC inayohusika na haki za binadamu,imeeleza kwamba uchunguzi wao umethibitisha mauaji ya watu wanane, wakiwemo watoto watatu wasio hatia, yalitukia tarehe 02 Januari katika kijiji kilichopo Goma, eneo la mashariki. Kwa mujibu wa MONUC mauaji haya yaliendelezwa na askari wa Jeshi la Taifa la Kongo.

Kadhalika tuliarifiwa kwamba baina ya tarehe 16 hadi 20 Januari, raia 30 waliuawa na wafuasi wa Jenerali Mtoro Laurent Nkunda katika kijiji cha Kalonge, kwa kisingizio kuwa walikwenda kutafuta hifadhi kwenye eneo linalodhibitiwa na wale ambao wafuasi wa Nkunda wanaamini ni adui.

Umopja wa Mataifa umeyakumbusha makundi yote haya dhamana walionayo kisheria juu ya hifadhi ya raia na ulazimu wa kuheshimu haki za binadamu na sheria za kiutu za kimataifa.