HLPF: Tanzania inasema iko mbioni kutokomeza njaa ifikapo 2030
HLPF: Tanzania inasema iko mbioni kutokomeza njaa ifikapo 2030
Wakati jukwaa la kisiasa la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa HLPF, kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs likielekea ukingoni hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, serikali ya Jamhui y Muungano wa Tanzania imesema iko mbioni kitimiza leongo namba 2 ya maendeleo endelevu SDG2, la kutokomeza njaa ifikapomwaka 2030.
Mweli amesema kuna mikakati mingi ambayo serikali ya Tanzania inaitekeleza hivi sasa kuhakikisha mlengo hilo linatimia ikiwemo kubadili mfumo wa kilimo, kutumia mbegu bora lakini pia kukumbatia teknolojia.
Kauli hiyo imetolewa na Gerald Geofrey Mweli, Katibu Mkuu kutoka wizara ya kilimo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipozungumza na Flora Nducha wa idhaa hii kuhusu ushiriki wake katika jukwaa hili.
Mahojiano haya yamefanyika katika Makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambako Bwana Gerald Geofrey Mweli anashiriki jukwaa hilo la wiki mmbili linlokunja jamvi wiki hii.